Chuo kikuu cha Alkafeel kinatoa ushauri wa tiba ya meno kwa kutumia mtandao

Maoni katika picha
Katika kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma za matibabu kwa wananchi wakati wote na katika mazingira yeyote, chuo kikuu cha Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya kimeanza kutoa ushauri wa kidaktari kwa kutumia mtandao wakati huu wa marufuku ya kutembea, kitivo cha meno katika chuo kikuu hicho kimeweka utaratibu wa kukutana na dokta kwa kutumia mtandao na kutoa ushauri wa kidaktari bure, huduma hii imeanza kutolewa kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya katika kipindi hiki kigumu.

Rais wa chuo Dokta Nurisi Muhammad Shahidi amesema kua: “Katika mazingira haya ambayo ni vigumu mwananchi kufika kwenye kituo cha afya, na mchango wa chuo chetu katika kupunguza shida za wanachi watukufu, tumetangaza kuanza kutoa huduma ya wataalamu wetu wakiwemo madaktari bingwa wa meno kukutana na raia na kutoa ushauri kwa njia ya mtandao”.

Akaongeza kua: “Kuna namba za simu zaidi ya 11 za wakufunzi ambao wanajibu maswali ya wananchi kwa haraka na kutoa maelekezo ya kidaktari”.

Akabainisha kua: “Tumetangaza aina za maradhi na namba za simu unazo takiwa kupiga kwenye mtandao maalum wa chuo pamoja na kwenye mitandao ya mawasiliano ya kijamii”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya imechukua hatua mbalimbali za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na inafanyia kazi maelekezo yanayo tolewa na idara ya afya, katika kiwango cha Ataba tukufu, mji mkongwe na mkoa kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: