Mkuu wa hospitali ya Hindiyya: Hakika kujenga kituo cha kuhudumia wagonjwa wa Korona sio jambo geni kwa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Mkuu wa hospitali ya Hindiyya Dokta Waathiq Hasanawi amesema kua; kama Ataba ilivyo ahidi, imeanza kujenga kituo cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona katika eneo la hospitali kuu ya Hindiyya.

Akaongeza kua: “Kituo hiki ni kwa ajili ya kupokea wagonjwa wa Korona katika mkoa mtukufu wa Karbala”.

Akabainisha kua: Ujenzi unafanywa wakati muhimu sana kwa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona na kulinda wananchi wa mkoa wa Karbala hususan wakazi wa wilaya ya Hindiyya.

Akasema: Tunatoa shukrani za dhati kwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi pamoja na watumishi wa Ataba kwa kusaidia haraka sekta ya afya.

Tambua kua Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya juhudi kubwa katika kupambana na maambuizi ya virusi vya Korona, na sasa imeanza ujenzi wa kituo cha kuhudumia wagonjwa wa Korona kwenye eneo la hospitali kuu ya Hindiyya, katika kiwanja chenye ukubwa wa (2m1500) jengo hilo litakua na vyumba 35 vya wagonjwa.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya ipo kwenye hatua za mwisho katika mradi wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona, kitakacho kua sehemu ya mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa mtukufu wa Karbala, kituo hicho kinajengwa kama zawadi kutoka hospitali ya rufaa Alkafeel katika mji wa Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala, na walio chukua jukumu la ujenzi huo ni kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: