Mwezi kumi na moja Shabani alizaliwa mwezi wa Alawiyya Ali Akbaru (a.s)

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo –mwezi kumi na moja Shabani- iliingia furaha katika nyumba ya Alawiyya kwa kuzaliwa mwezi mtukufu Ali Akbaru (a.s), alikua mtukufu miongoni mwa watukufu.

Nyota yake iliangaza katika jangwa la Twafu alipokua akipigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu chini ya baba yake bwana wa mashahidi Imamu Hussei (a.s).

Hadhi yake: Ali Akbaru anahadhi kubwa kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), hilo linaonekana wazi pale alipotoka kwenda kupigana katika siku ya Ashura baada ya kuruhusiwa na baba yake Imamu Hussein (a.s), Imamu alimuangalia kisha akalia halafu akainua mikono juu akasema: (Ewe Mola nakushuhudia watu hawa amewatokea kijana anayefanana zaidi na Mtume mtukufu sura, umbo na kuongea, tulikua tukimkumbuka Mtume wako tunamuangalia kijana huyu, ewe Mola wanyime baraka za ardhi na uwatenganishe wawe makundi makundi wala usiwaridhie milele, hakika wametwita kutunusuru kisha wametufanya maadui na kutuuwa).

Hiyo ndio nafasi ya Ali Akbaru (a.s) kwa baba yake Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s), katika ziara tunamkuta Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Kwa haki wewe na mama kutokana na aliyechinjwa na kuuwawa bila kosa), makutano ni kwa Mwenyezi Mungu ewe bwana wangu ewe Ali Akbaru ukiwa katika nafasi yako tukufu.

Sifa zake: Alikua mzuri mwenye muonekano wa kupendeza alikua anafanana zaidi na babu yake Mtume Muhammad (s.a.w.w) tabia umbo na kuongea, alikua shujaa asiye ogopa vita, ushujaa wake alirithi kutoka kwa babu yake kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s), alikua anakila sifa nzuri kama walivyokuwa wazazi wake watakasifu, alijulikana kwa zuhudi, ibada, kukirimu wageni na kusaidia masikini.

Kaburi lake tukufu lipo upande wa miguu ya kaburi la baba yake Imamu Hussein (a.s), imesuniwa wakati wa ziara kusimama upande wa miguuni, na ziara ya Ali bun Hussein utasoma hivi: (Amani iwe juu yako ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, amani iwe juu yako ewe mtoto wa Nabii wa Mwenyezi Mungu, amani iwe juu yako ewe mtoto wa kiongozi wa waumini, amani iwe juu yako ewe mtoto wa Hussein Shahidi, amani iwe juu yako ewe shahidi, amani iwe juu yako ewe mdhulumiwa na mtoto wa mdhulumiwa, Mwenyezi Mungu awalaani walio kuuwa, na awalaani walio kudhulumu, na awalaani watakao sikia hayo (dhulma ulizo fanyiwa- kisha wakaridia).

Amani iwe juu yake siku aliyo zaliwa na siku aliyo uwawa na siku atakayo fufuliwa kua hai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: