Kutokana na kuongezeka maombi: Idara ya ushonaji katika Atabatu Abbasiyya imeshona zaidi ya barakoa (maski) elfu (40).

Maoni katika picha
Idara ya ushonaji katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeshona zaidi ya barakoa (maski) elfu (40) baada ya kuongeza ushonaji kutokana na ukubwa wa mahitaji kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Korona.

Koingozi wa idara Ustadh Abdu-Zahura Daud Salmaan amesema kua: “Tangu siku za kwanza tulizo anza kushona barakoa (maski) na kufungua idara maalum ya kazi hiyo, tumekua tukiongeza utendaji kutokana na mahitaji ya Ataba ya barakoa (maski) hizo, ambazo inazigawa bure kama sehemu ya kuunganisha nguvu ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, na hisia kubwa za uzalendo wa taifa hili”.

Akaongeza: “Mafundi wa ushonaji wanashona kwa juhudi kubwa, utawakuta wanafanya kazi kama nyuki kila mtu yupo bize na kazi yake, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tunatarajia kuongeza uzalishaji katika siku zijazo kama hali itaendelea kua kama ilivyo –Allah atuepushie-”.

Akasisitiza kua: “Vitambaa tunavyo tumia vimepasishwa na idara ya afya ya mkoa wa Karbala na vimepimwa na idara ya madaktari wa Ataba tukufu, matokeo ya vipimo yamethibitisha kua ni aina bora, na ushonaji unafanywa kwa kuzingatia maelekezo ya iadara ya afya”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya imechukua hatua mbalimbali za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na inafanyia kazi maelekezo yanayo tolewa na idara ya afya, ushonaji wa barakoa (maski) ni moja ya harakati zake za kupambana na upungufu wa vifaa hivyo katika soko na kwenye vituo vya afya, kutokana na ukubwa wa matumizi yake kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: