Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa pole kwa kufiwa na muimbaji wa Husseiniyya bwana Jaasim Nawini Torijawi

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu inatuma salam za rambirambi kwa kufiwa na mtumishi wa Hussein (a.s) muimbanji mkubwa mzee Jaasim Nawini Torijawi, aliye fariki asubuhi ya leo Jumapili mwezi (11 Shabani 1441h) sawa na tarehe (5 Aprili 2020m), tamko la rambirambi linasema:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

(Ewe nafsi uliyetulia * Rejea kwa Mola wako ukiwa umeridhia na kuridhiwa * Ingia katika waja wangu * na india katika pepo yangu).

Hakika wale walioitikia wito usemao: (Huisheni mambo yetu Mwenyezi Mungu amrehemu atakaehuisha mambo yetu)

Hakika wale waliobeba bendera ya Hussein (a.s) bendera ya haki na mwanga wa uongofu anapo andoka mmoja wao kwenda katika ulimwengu wa akhera huliliwa na viumbe wa duniani..

Kwa huzuni kubwa, uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unatuma rambirambi kwa kufiwa na mtumishi wa mimbari ya Hussein (a.s) shekh muimbaji mzee Jaasim Nawini Torijawi, aliyekufa asubuhi ya leo siku ya Jumapili mwezi (11 Shabani 1441h) sawa na tarehe (5 Aprili 2020m) baada ya safari ndefu ya kumtumikia Imamu Hussein (a.s), Mwenyezi Mungu amtie katika rehema zake na amuweke mahala pema peponi na amfufue pamoja na aliokua anawapenda na kuwatawalisha, awe pamoja na Muhammad na watu wa nyumbani kwake watakasifu (a.s), Mwenyezi Mungu aipe subira na utulivu familia yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: