Kutoka Atabatu Abbasiyya.. muwakilishi wa shirika la afya la kimataifa hapa Iraq: amesema kua Marjaa Dini mkuu amerahisisha jukumu letu la kupambana na virusi vya korona kutokana na maelekezo na nasaha zake

Maoni katika picha
Dokta Ad-ham Rishadi Ismaili muwakilishi wa shirika la afya la kimataifa hapa Iraq amesema kua, hakika Maelekezo na nasaha za Marjaa Dini mkuu, umesaidia jukumu letu la kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona hapa Iraq.

Amesema hayo alipo tembelea Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya Adhuhuri ya Jumapili mwezi (11 Shabani 1441h) sawa na tarehe (5 Aprili 2020m), na akakutana na katibu mkuu pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi pamoja na mkuu wa Hospitali ya rufaa Alkafeel.

Mwishoni mwa ziara hiyo, dokta Ad-ham Rishadi Ismaili akauambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mimi nimetembelea mkoa wa Karbala nikiwa na amani kutokana na hatua zilizo chukuliwa za kujikinga na virusi vya Korona ambavyo vinasumbua sehemu kubwa ya dunia, namshukuru Mwenyezi Mungu hapa Iraq hali sio mbaya sana, wakati wowote tishio la virusi hivyo linaweza kuisha, lakini ni muhimu kuendelea kuchukua kila aina ya tahadhari”.

Akaongeza kua: “Wizara ya afya ya Iraq imeweka kanuni na utaratibu mzuri sana wa kujikinga na maambukizi ya Korona, wananchi wanatekeleza vizuri maelekezo hayo pamoja na kuwepo kwa watu wachache wasio tekeleza baadhi ya maagizo, kupitia mimbari yenu nawaambia wairaq kua mnatakiwa kufuata maelekezo ya wizara ya afya kwa ajili ya kuhakikisha tunatoka salama katika mtihani huu”.

Akasema: “Nafurahi sana hatua zinazo chukuliwa na Ataba tukufu za kupuliza dawa chini ya maelekezo ya wizara ya afya, baada ya kumaliza mtihani huu natarajia iwepo miradi shilikishi baina yetu na Atabatu Abbasiyya na tuendelee kuwasiliana, shirika la afya la kimataifa linathamini mchango wa Marjaa Dini na Ataba tukufu za Iraq, kwa kujenga uwelewa wa mambo ya afya pamoja na Dini”.

Akamaliza kwa kusema: “Tunamshukuru sana Marjaa Dini mkuu kwa kushirikiana na wizara ya afya, kupitia khutuba, maelekezo na nasaha ambazo zimerahisisha sana kazi yetu, tunamuomba Mwenyezi Mungu atuondoshee balaa hili hapa Iraq na kila sehemu ya dunia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: