Kituo cha (Ruhamaau-Bainahum) kinapuliza dawa katika mitaa ya mafakiri

Maoni katika picha
Juhudi za watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu zinaongezeka kila siku katika kuendelea kupuliza dawa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, hivi karibuni kituo cha (Ruhamaau-Bainahum) chini ya kitengo cha malezi na elimu kimeanzisha opresheni ya kupuliza katika maeneo yanayo kaliwa na mafakiri na katikati ya mji wa Karbala, pamoja na kwenye nyumba zinazo kaliwa na watoto wanao lelewa na kituo hicho.

Kazi hiyo inafanywa na kamati iliyo undwa na kituo hicho pamoja na vijana wa Karbala, wanapuliza dawa kwenye mitaa inayo kaliwa na mafakiri pamoja na katikati ya mji na kwenye nyumba za familia za watoto wanao lelewa na kituo hicho, tena wanatumia vifaa maalum vilivyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kutoka katika shirika la Khairul-Juud, vinavyo endana na mazingira ya maeneo hayo sambamba na kukidhi vigezo vya wizara ya afya.

Nayo Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa beji la vifaa vya afya kwa kila familia ya mtoto anayehudumiwa na kituo hicho.

Wakazi wa maeneo hayo wameishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na kituo cha (Ruhamaau-Bainahum) kwa kazi hiyo, ambayo ni sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya kamati ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya na idara ya afya ya mkoa wa Karbala.

Tambua kua mradi wa (Ruhamaau-Bainahum) ni mradi wa kulea watoto wanao ishi katika mazingira magumu –waliokosa malezi ya familia- na unafadhiliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya inaendesha opresheni ya kupuliza dawa chini ya kamati maalum ya kujikinga na maambukizi ya Korona katika maeneo yanayo zunguka Ataba, mji mkongwe na barabara zote zinazo ingia katika mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: