Katika kukagua miradi inayo tekelezwa.. kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu anakagua utendaji wa shirika la Khairul-Juud

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ametembelea shirika la Khairul-Juud, na kukagua utendaji wao katika wakati huu ambao wameongeza uzalishaji kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya wananchi na vituo vya afya katika bidhaa za barakoa na visafishio, Mheshimiwa amefuatana na makamo katibu mkuu wa Ataba tukufu na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na raisi wa kitengo cha miradi ya kihandisi.

Mjumbe wa kamati ya uongozi katika Atabatu Abbasiyya Ustadh Jawadi Hasanawi amesema kua: “Ziara hii ni sehemu ya ufuatiliaji wa miraji ya Ataba tukufu, hususan inayotoa huduma muhimu katika kipindi hiki ambacho tunapambana na maambukizi ya virusi vya Korona, miongoni mwa miradi muhimu kwa sasa ni shirika la Khairul-Juud linalo tengeneza barakoa na visafishio vinavyo hitajiwa na kila mtu katika jamii, pamoja na taasisi za afya”.

Akaongeza kua: “Bidhaa zinazo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud zimekidhi vigezo vyote vya kiafya, na zinakidhi mahitaji ya taasisi za afya za Iraq, kwa hiyo ni muhimu kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa kiwango kikubwa kadri itakavyo wezekana”.

Naye mkuu wa kamati tendaji ya shirika hilo Mhandisi Maitham Bahadeli amesema kua: “Mheshimiwa Sayyid Swafi ametembelea shirika hili kwa ajili ya kuangalia namna ya kuondoa changamoto za kiutendaji”.

Akaongeza kua: “Mheshimiwa ameangalia uzalishaji na mitambo inayo tumika sambamba na kuangalia namna ya kuiboresha kwa ajili ya kuongeza uwezo wa uzalishaji, pamoja na miradi ya tafiti inayo fanywa na shirika hili”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: