Zaidi ya vikapu elfu (35) vya chakula: Vimetolewa na Mawakibu za waasit katika kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo

Maoni katika picha
Miongoni mwa wawakilishi wanao saidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo ni mawakibu za mkoa wa Waasit, chini ya kitengo cha mawakibu katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, zilianza kutoa misaada tangu siku za kwanza za kutolewa kwa maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na kuanza opresheni ya Takaaful, inayo husu kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo ambao wameathiriwa na marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Korona hapa Karbala na nchi nzima kwa ujumla, hadi sasa wamesha gawa zaidi ya vikapu (35,000) vya chakula, na bado wanaendelea kugawa.

Kwa mujibu wa kiongozi wa mawakibu hizo bwana Daakhil Anidi Quraishi, amesema: “Mawakibu zetu zinafanya kazi ya kugawa vikavu vya chakula wakati wote na kila mahala bila kupumzika, kama zilivyo weza kusimama pamoja na wapiganaji wakati wa vita dhidi ya magaidi wa Daesh, aidha ni sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu yaliyo saidia kushinda vita dhidi ya magaidi hao, leo mawakibu hizo zimesimama kuitikia wito wa Marjaa kwa mara nyingine, wa kuwasaidia mapambano dhidi ya virusi vya Korona, na kuimarisha mshikamano na ushirikiana katika jamii”.

Akafafanua kua: “Mawakibu zinafanya kazi ya kugawa chakula kila siku kuanzia asubuhi hadi usiku, katika kusaidia familia zenye kipato kidogo”.

Akabainisha kua: “Kutokana na wingi wa maombi yanayo tufikia tumegawa majukumu ya kugawa chakula kulingana na jografia ya kila maukibu, kama tukichelewa kuifikia familia yeyote yenye uhitaji jambo hilo litakua liko nje ya uwezo wetu, tunazihakikishia familia zote kua tutazifikia na tutagawa zaidi ya kikapu kimoja kwa familia kama janga hili likiendelea -Allah atuepushie-”.

Akasisitiza kua: “Sehemu tulizo zifikia na kugawa misaada ya chakula ni: (kata ya Waasit, kata ya Shekh Sa’di, wilaya ya Nu’maniyya, wilaya ya Swawirah, wilaya ya Zubainiyya, kata ya Shahimiyya, wilaya ya Aziziyya, kata ya Taju-Dini, kata ya Dabuni).

Kumbuka kua Marjaa Dini mkuu alitoa wito kwa mawakibu Husseiniyya zisaidie familia za watu wenye kipato kidogo, hayo yapo kwenye tamko lake lisemalo: (Inazipasa mawakibu Husseiniyya zilizo simama imara kuwasaidia wapiganaji wakati wa vita dhidi ya magaidi wa Daesh, zijitokeze kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo wakati huu mgumu wa marufuku ya kutembea).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: