Kamati inayo simamia majengo ya shekh Kuleini linaendelea na kazi ya kupuliza dawa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona

Maoni katika picha
Kamati inayo simamia majengo ya Shekh Kuleini yaliyopo katika barabara ya (Karbala – Bagdad) inaendelea na opresheni ya kupuliza dawa kwa ajili ya kujikinga na mambukizi ya virusi vya Korona.

Kiongozi wa kamati hiyo, bwana Ali Mahdi Abbasi Swafi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika upuliziaji wa dawa upo katika mkakati wa Atabatu Abbasiyya, unaohusisha kupuliza dawa ndani ya kumbi za Ataba na sehemu inayo zunguka mji mkongwe, kwa kutumia vifaa tulivyo pewa na shirika la Khairul-Juud na kufuata vigezo vyote vilivyo tolewa na wizara ya afya ya Iraq na shirika la afya la kimataifa”.

Akaongeza kua: “Hakika kazi ya kupuliza dawa inaendelea kwa wiki ya tatu mfululizo, majengo yote hupuliziwa dawa”.

Akabainisha kua: “Kazi hii hufanywa chini ya kauli mbiu isemayo (kinga ni bora kuliko tiba) inalenga kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, pia tunajenga uwelewa kuhunu namna ya kujikinga na virusi vya Korona kwa kugawa vipeperushi na kushirikiana na taasisi za afya sambamba na kufuata maelekezo yote yanayo tolewa na idara ya afya”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inamkakati maalum wa kupuliza dawa chini ya kamati maalum iliyo undwa kwa jukumu hilo, inahusika na kupuliza dawa maeneo yote yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya na mji mkongwe pamoja na barabara zote za mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: