Kituo cha uchapishaji na usambazaji Darul-Kafeel kinaendelea na kazi ya kutengeneza vifaa vinavyo tumika kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona

Maoni katika picha
Kituo cha uchapishaji na usambazaji Darul-Kafeel kinaendelea na kazi ya kutengeneza vifaa vinavyo tumika kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, kama sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kusaidia sekta ya afya, aidha kutokana na maelekezo ya moja kwa moja ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya kuhusu ulazima wa kuendelea kufanya tafiti katika kipindi hiki kigumu ambacho taifa linapitia kwa sasa.

Kiongozi wa Darul-Kafeel Ustadh Farasi Haakim ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Darul-Kafeel inaendelea kutengeneza kifaa cha kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, kifaa hicho kinatumiwa na wahudumu wa afya na askari kujikinga na maambukizi ya virusi vya korona wakati wa kufanya majukumu yao, kimetengenezwa viruri na kimekidhi vigezo vyote vinavyo hitajika na wizara ya afya, kina kifaa cha kukinga uso na sehemu ya sponji (pvs) inayo tumika kama ngao, hiki ni miongoni mwa vifaa bora zaidi vya kujikinga, virusi vya Korona haviwezi kupenya katika kifaa hicho, pia kinakinga macho na kinaweza kutumiwa zaidi ya mara moja”.

Akabainisha kua: “Mara ya kwanza tulitengeneza vifaa (500) ambavyo tulivigawa kwa wahudumu wa afya, na hivi sasa tunatengeneza vifaa (1000) kwa siku, na tunatarajia kuongeza uzalishaji zaidi Insha-Allah”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya inaendesha opresheni ya kupuliza dawa chini ya kamati maalum ya kujikinga na maambukizi ya Korona katika maeneo yanayo zunguka Ataba, mji mkongwe na barabara zote zinazo ingia katika mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: