Kwa video: Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ametembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambuizwa virusi vya Korona katika hospitali ya Hindiyya

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar ametembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusu vya Korona, unaojengwa katika eneo la hospitali ya Hindiyya chini ya ufadhili wa Atabatu Abbasiyya.

Ametembelea kuangalia maendeleo ya kazi na kuwahimiza watekelezaji wa mradi huo wahakikishe unakamilika kwa wakati uliopangwa na viwango vinavyo takiwa na wanufaika.

Kumbuka kua mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu walianza ujenzi huo mwezi (6 Shabani 1441h) sawa na tarehe (31 Machi 2020m) katika uwanja wa hospitali ya Hindiyya, ukubwa wa kiwanja hicho ni (2m1500) jengo hilo litakua na vyumba (35) vya wagonjwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: