Ziara kwa niaba katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa binadamu na ziara maalum ya nusu ya mwezi wa Shabani.

Maoni katika picha
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussawi amesema kua kuna kikosi cha Abulfadhil Abbasi (a.s), kinacho undwa na masayyid na wanafunzi wa dini pamoja na kundi la wafanya kazi wa Ataba, kinacho fanya ziara ya Imamu Mahadi na ya nusu wa mwezi wa Shabani katika haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa niaba.

Akaongeza kua: “Wakati huohuo watafanya ziara maalum kwaniaba ya watumishi wa afya na askari wanaopambana kulinda wananchi dhidi ya virusi vya Korona”.

Akabainisha kua: Ukizingatia kua wakati huu ni wa kuadhimisha kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda tutanyanyua mikono na kusoma surat Fatha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Hashdi Shaábi na wanajeshi wa serikali, pamoja na waliokufa kwa maradhi ya Korona.

Akasisitiza kua: Tunazingatia maagizo yote ya kiafya yanayo tolewa na sekta za afya, kwa ajili ya kulinda usalama wa jamii na kuheshimu maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, kama vile kuvaa barakoa (maski), soksi za mikononi na kuweka umbali unaotakiwa kati ya mtu na mtu”.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atukubalie ibada zote tunazo fanya katika mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: