Katika kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu yanayo himiza kuheshimu maagizo ya serikali na wizara ya afya katika kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, Atabatu Abbasiyya inaendeleza harakati zake kwa kutumia njia za mitandao.
Hivyo idara ya Quráni kitengo cha wanawake/ ofisi ya maelekezo ya kidini chini ya ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu imeanzisha harakati za kiroho kwa njia ya intanet ili watu waendelee kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa pamoja wakiwa mbali, kuhusu program hiyo tumeongea na Ustadhat Fatuma Mussawi kiongozi wa ofisi hiyo amesema kua: Hakika upande wa kiroho ni muhimu sana katika kukomaza nafsi kwani madaktari wanasema hofu na wasiwasi vina athari mbaya kwa mwanadamu, ni miongoni mwa sababu za kushusha uwezo wa kujikinga na virusi vya Korona, hivyo tunahakikisha tunatuliza nyoyo za wananchi kwa kusoma Quráni, kumbuka Mwenyezi Mungu anasema (Tambua! Nyoyo hutulia kwa kumtaja Mwenyezi Mungu).
Akaongeza kua: Hakika tunatakiwa kurudi kwa Mwenyezi Mungu wakati wa mitihani, yeye ndiye mfalme wa mbinguni na ardhini, anauwezo wa kuondoa mabalaa na maradhi.
Akasema: wakati huu wa marufuku ya kutembea tumesha soma khitima arubaini kwa njia ya masafa na leo tutaanza usomaji wa awamu nyingine.
Kumbuka kua pamoja na kusoma Quráni, tunasoma pia masomo ya Fiqhi na Aqida sambamba na kuweka kipengele cha maswali na mashindano.