Idara ya shule za Dini za wasichana Alkafee inatangaza shindano katika kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa wa Imamu Mahdi (a.f)

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu wa zama (a.f) na kutokana na hadithi ya kiongozi wa waumini (a.s) isemayo: (Utukufu wa mtu ni kwa elimu na akili yake sio mali na ukoo), idara ya shule za Dini za wasichana Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inatangaza shindano kwa wasichana tu, liitwalo (Njia ya uwokovu).

Shindano hilo litakua na maswali ya Fiqhi, Aqida pamoja na masomo mengine, litaanza siku ya Ijumaa (16 Shabani 1441h) sawa na tarehe (10 Aprili 2020m), litaendelea kwa muda wa siku tano.

Kila mtu atakaeshiriki atapewa zawadi, ikiwa ni pamoja na kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kusoma dua ya Tawasul na ziara Ashura, pia kutakua na zawadi za kutabaruku kutoka katika malalo takatifu kwa watu hamsini wa kwanza.

Kumbuka kua shindano hili litafanywa kwa njia ya mtandao, kama itakavyo tangazwa hapo baadae.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: