Ufundishaji wa Quráni kwa njia ya mtandao ni harakati ya idara ya Quráni ya wasichana

Maoni katika picha
Ufundishaji wa Quráni kwa njia ya mtandao ni harakati ya idara ya Quráni ya wasichana…

Mawasiliano ya kimtandao ni njia kubwa ya kuendeleza ufundishaji, ndio njia inayotumiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuendesha harakati zake wakati huu wa kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, ambapo kuna maelekezo yaliyo tolewa na wizara ya afya na Marjaa Dini mkuu akahimiza kuyaheshimu.

Katika mazingira haya, idara ya Quráni/ ofisi ya maelekezo ya kidini ya wanawake chini ya ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanzisha ratiba ya kiroho (ya usomaji wa Quráni ukiwa mbali) ambapo kutakua na kisomo cha pamoja huku wasomaji wakiwa mbali, ili kuhakikisha usomaji wa Quráni unendelea pomoja na kuwepo kwa marufuku ya mikusanyiko.

Ustadhat Fatuma Mussawi kiongozi wa idara hiyo amesema kua: “Tumefanya kila tuwezalo kuhakikisha tunaendelea kuwasiliana na kusomesha Quráni kwa njia ya masafa (mtandao) wakati wa kipindi hiki cha marufuku ya kutembea”.

Akaongeza kua: “Lengo kuu ni kuhakikisha wasichana wanaendelea kusoma Quráni na mambo yenye manufaa kwao duniani na akhera”.

Kumbuka kua idara tajwa imekamilisha ratiba ya (usomaji wa Quráni ukiwa mbali) zaidi ya mara arubaini tangu ilipo wekwa marufuku ya kutembea hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: