Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu amepongeza ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona hapa Karbala

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar amepongeza kazi kubwa inayofanywa na watumishi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi ya kujenga kituo cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona, kazi ambayo inakaribia kukamilika, wapo katika hatua za mwisho, akasema kua mafanikio hayo sio jambo geni kwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Ameyasema hayo alipo tembelea mradi huo akiwa na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya na kiongozi mkuu wa hospitali ya rufaa ya Alkafeel, kwa ajili ya kuangalia hatua za mwisho za ujenzi wa mradi huo.

Watendaji wa mradi huo wamemueleza katibu mkuu na kamati kuu ya uongozi kuhusu mafanikio ya mradi huo, pamoja na hatua za mwisho katika ujenzi huo, wakaahidi kua saa chache zijazo watakamilisha kila kitu na kukabidhi jengo kwa uongozi wa mji wa Imamu Hussein (a.s).

Kumbuka kua ujenzi huu umefanywa kutokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu yanayo himiza kusaidia sekta ya afya, na mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kulinda jamii kutokana na virusi vya Korona, mafundi wa kitenfo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu walianza kazi mara moja baada ya kauli ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, wakaanza kujenga kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mji wa Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala, chini ya usimamizi wa idara ya madaktari wa Ataba tukufu na hospitali ya rufaa Alkafeel, kama sehemu ya kuchukua tahadhari iwapo likitokea tatizo hilo –Allah atuepushie-.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: