Sherehe za kuingia siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu Imamu wa zama hizi (a.f), ambaye kumbukumbu hiyo inasadifu siku ya leo mwezi (14 Shabani 1441h), dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) limepambwa chupa za mauwa mazuri ambayo yamezunguka eneo lote la dirisha na kufanya mazingira kuwa maziru sana kiasi ambacho yanatia furaha katika nyoyo za waumini.
Kazi ya kuweka mauwa hayo imefanywa na watumishi wa idara ya vitalu vya Alkafeel, sambamba na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, kikosi cha masayyid ndio waliobeba mauwa hayo na kuyaweka juu ya dirisha, kabla ya kufanya hivyo walianza kwa kusoma ziara na kuomba dua, Mwenyezi Mungu awape afya na amani kwa baraka za anaeadhimishwa kuzaliwa wake.
Mauwa na mabango hayo hayajawekwa ndani ya malalo peke yake, bali yamewekwa hadi nje ya malalo, milangoni, kwenye korido na katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, sehemu zote zinawakawaka kutokana na uzuri wa mauwa hayo.