Kumbukumbu ya miaka 1186 tangu kuzaliwa kwa amani ya viumbe wa ardhini na tumaini aliye ahidiwa

Maoni katika picha
Historia ya uzawa mtakatifu

Alizaliwa (a.s) kwenye nyumba ya baba yake Imamu Hassan Askariy (a.s) katika mji wa Samaraa mwishoni mwa usiku wa Ijumaa mwezi kumi na tano Shabani, nao ni usiku mtukufu ambao imesuniwa kuuhuisha kwa kufanya ibada na kufunga mchana wake kwa mujibu wa riwaya tukufu.

Alizaliwa mwaka wa (255h) kwa mujibu wa riwaya mashuhuri, kuna riwaya chache zinazo sema kua alizaliwa mwaka wa (256h) na zingine zinasema mwaka wa (254h) pamoja na kukubaliana siku aliyo zaliwa, lakini tarehe sahihi ni ile ya kwanza, Imamu Mahdi (a.s) aliishi miaka michache kabla ya kufariki baba yake Imamu Hassan Askariy (a.s), aidha riwaya nyingi zinasema kua alizaliwa siku ya Ijumaa mwezi kumi na tano Shabani pamoja na kutofautiana miaka alio zaliwa, kama tukiangalia miaka inayo tajwa kuwa alizaliwa tutakuta mwaka ambao mwezi kumi na tano Shabani inasadifu siku ya Ijumaa ni mwaka wa (255h) peke yake.

Tofauti kama hii ni jambo la kawaida imetokea pia katika tarehe za kuzaliwa na kufariki kwa baba zake watukufu hata babu yake Mtume (s.a.w.w) bila kuathiri kuthibiti kuzaliwa kwao (a.s), kutofautiana kwa tarehe za kuzaliwa kwao kunalinda matukio hayo matakatifu.

Mazingira ya kuzaliwa kwake

Riwaya zinazo zungumzia mazingira ya kuzaliwa kwake (a.s) zinasema kua, mzazi wake Imamu Hassan Askariy (a.s) alificha sana mazingira ya kuzaliwa kwake, Imamu Hassan Askariy (a.s) alimuambia shangazi yake bibi Hakimah mtoto wa Imamu Jawaad abakie nyumbani kwake usiku wa mwezi kumi na tano Shabani, na akamuambia kua katika usiku huo atazaliwa mtoto wake na hoja ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, akamuuliza nani mama wa mtoto huyo, akamuambia kua ni bi Narjisi, akaenda kwake akamkagua lakini hakuona athari ya mimba, akarudi kwa Imamu akamuambia kua hana athari ya mimba, Imamu akatabasamu na akamuambia, mfano wake ni sawa na mama wa Nabii Mussa (a.s), haikuonekana athari ya mimba yake wala hakuna yeyote aliyetambua ujauzito wake hadi wakati wa kujifungua kwake, kwa sababu Firáuni aliweka ulinzi mkali kwa wajawazito wote wa bani Israeel kwani alikua anaogopa kuzaliwa kwa Nabii Mussa (a.s) aliye bashiriwa kwake, hivyo alikua anawauwa watoto wa kiume na kuwanyanyasa watoto wa kike, hivyo ndio ilivyokua kwa Imamu Mahdi (a.s), mfalme wa bani Abbasi alikua anafuatilia kwa karibu kuzaliwa kwake kwani alikua amesha bashiriwa katika hadithi tukufu.

Kutokana na riwaya hizo inaonyesha waki kua alizaliwa karibu na wakati wa Alfajiri, kwa hakika kulikua na umuhimu mkubwa wa kuficha mazazi yake, kwani wapepelezi wa mfalme mara nyingi wakati huo huwa wapo kwenye usingizi mzito, pia riwaya zinaonyesha kua mazazi yake hayakuhudhuriwa na mkunga mwingine zaidi ya bibi Hakimah ambaye pia hakujua kwa uhakika wakati wa kujifungua.

Hadithi zilizo tangulia zinaonyesha sababu ya kuficha siku ya kuzaliwa kwake (a.s), sababu hizo hizo ndio zilisababisha siku ya kuzaliwa Nabii Mussa (a.s) ifichwe pia, ambayo ni kumlinda anaezaliwa asiuwawe na kutimiza hoja ya Mwenyezi Mungu mtukufu kwa waja wake na kumfanya atekeleze wajibu wake uliokua ni kuwaokoa bini Israeel pamoja na kupambana na uovu wa Firáuna kwa Nabii Mussa (a.s), na kumaliza dhulma na kuweka haki na uwadilifu pamoja na kuufanya uislamu uwe juu ya dini zote chini ya uongozi wa Imamu Mahdi (a.f).

Jambo hilo walikua wanalitambua vizuri viongozi waovu kutokana na riwaya zinazo mzungumzia, Firáuni wa zama hizo alikua anajua kuwa atazaliwa muokozi wa bani Israeel, ambaye ni Mussa (a.s) atakaetokana na wao, ndio akaamua kuua watoto wote wakiume waliokua wanazaliwa na bani Israeel ili kuzuwia asipatikane, hivyo hivyo ndio walivyokua bani Abbasi, walijua kua Mahadi aliye ahidiwa atatokana na kizazi cha Fatuma (a.s), naye ni Imamu wa kumi na mbili katika Maimamu wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), hadithi za Mtume (s.a.w.w) zinazo bashiri kuzaliwa kwa Imamu Mahadi (a.f) zilikua zinajulikana sana katika jamii ya waislamu, tena ziliandikwa na wanachuoni wa hadithi kwa miongo mingi kabla ya kuzaliwa kwake, pia walikua wanajua wazi kua Imamu Hassan Askariy (a.s) ndio Imamu wa kumi na moja, kwa hiyo walifanya kila wawezale kuzuwia kuzaliwa kwa Mahadi aliye ahidiwa kwa kuhakikisha Imamu Hassan (a.s) hapati mtoto wa kiume.

Kutokana na usahihi wa hadithi hizo ilitosha kuwa sababu inayo wasukuma kumuuwa, pia hawakuwa na ushahidi wa kuonyesha kua hadithi hizo zinahusu kizazi chao, bali ushahidi wote ulionyesha kua zinahusu maimamu kumi na mbili watokanao na kizazi cha Mtume (s.a.w.w).

Imepokewa kutoka kwa Imamu Hassan Askariy (a.s) na Shekh aliye ishi katika zama zake Fadhili bun Shadhani:

Anasema: Imesimuliwa na Abdullahi bun Hussein bun Saádi Kaatibu anasema, Abu Muhammad Imamu Askariy (a.s) anasema: “Bani Umayya na bani Abbasi wameweka panga zao juu yetu kwa sababu mbili: kwanza walikua wanatambua wazi kua hawana haki ya ukhalifa, wakawa wanaogopa tusidai haki hiyo na kuurudisha ukhalifa mahala pamke, jambo la pili walikua wanatambua wazi kuwa utawala wa kitwaghuti na dhulma utaondolewa na kiongozi anayetokana na sisi, walikua wanajua wazi kuwa wao ni viongozi waovu na madwalimu, ndio maana wakaamua kuwauwa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) na wakataka kuangamiza kizazi chake ili wazuwie kuzaliwa kwa Imamu Mahadi (a.f) au wamuuwe, Mwenyezi Mungu akamlinda na mauwaji yao kama anavyo sema (Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake japokua makafiri watachukia)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: