Mkuu wa askari wa kikosi cha kwanza katika mji wa Karbala amesema: Tunakishukuru kikosi cha Abbasi tutaendelea kuwadhania vizuri

Maoni katika picha
Mlikua ngome imara dhidi ya magaidi wa Daesh

Leo mmekua ngome imara dhidi ya ugonjwa wa Korona

Imekuja nafasi yenu

Zibarikiwe juhudi zenu

Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji asubuhi ya Alkhamisi ya leo mwezi (15 Shabani 1441h) sawa na tarehe (9 Aprili 2020m) kimefanya gwaride ya kijeshi pamoja na kupewa bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na baadhi ya zawadi zingine ikiwemo bendera ya Iraq na mauwa, kwa kikosi cha kwanza cha afya kinacho fanya kazi katika mji wa Imamu Hussein (a.s).

Kiongozi wa mji wa Imamu Hussein (a.s) Dokta Swabahu Husseini amekishukuru kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wakati wa gwarige la kijeshi na kuwapa mauwa na zawadi ya bendera ya Abulfadhil Abbasi kwa kazi kubwa wanazo fanya.

Akaongeza kua: “Sisi ni wadaiwa wa vikosi vya usalama hususan kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji ambacho kinatupa huduma bora, na kimetupa majukumu makubwa baada ya kupeba bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mimi na wenzangu katika kikosi cha kwanza tutaendelea kushirikiana vizuri na Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na raia wote, ugonjwa huu utaisha kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kutokana na mshikamano wa askari pamoja na madaktari na kila anayeshiriki katika mapambano haya kwa namna yeyote ile hadi wale wanao saidia familia za wahitaji (mafakiri na watu wenye kipato kidogo).

Kumbuka kua kikosi cha wapiganaji cha Abbasi kimefanya kwaride la kijeshi kuwapongeza wawakilishi wake na kuwakabidhi bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na zawadi zingine ikiwemo bendera ya Iraq na mauwa, kama sehemu ya kuthamini kazi wanazo fanya na kusherehekea mazazi ya Imamu wa zama (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: