Idara ya mapambo na miti imeanza kuhamisha miche (1870) ya aina tofauti na kuipelekea katika mradi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona hapa Karbala

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya mapambo na miti chini ya kitengo cha utumishi wameanza kupanda aina mbalimbali za mauwa na miti katika kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona.

Kiongozi wa idara hiyo Mhandisi Ahmadi Mahmudu ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tumeandaa miche ya aina tofauti kwa ajili ya kupandwa kwenye kituo hiki, kutokana na umuhimu wa miche hiyo kwenye kituo hiki”.

Akaongeza kua: “Hatujaishia kupanda miche hiyo milangoni na kwenye uwanja wa mbele peke yake, bali tumeweka miche kadhaa hadi sehemu ya ndani, kwenye kumbi kuu na vyumba vya wagonjwa”.

Akabainisha kua: “Tutapanda miche (1500) ya mauwa na miti katika uwanja wa mbele, na miche (250) ya aina zingine za miti, pamoja na zaidi ya miche (120) itawekwa ndani ya kituo”.

Kumbuka kua mafundi wanaofanya kazi katika kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, walianza ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona chini ya maelekezo ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, katika mji wa Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala na katika hospitali ya Hindiyya, kama sehemu ya kujiandaa kupokea wagonjwa wa virusi hivyo kama wakitokea (Allah atuepushie).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: