Baada ya siku (15) tu: Kituo cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona kimekamilika

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Ijumaa ya leo mwezi (16 Shabani 1441h) sawa na tarehe (10 Aprili 2020m), wamekamilisha ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walioambukizwa virusi vya Korona kwenye mji wa Imamu Hussein (a.s) katika mkoa wa Karbala, chini ya usimamizi wa idara ya madaktari wa Ataba na hospitali ya rufaa Alkafeel na ufunguzi wa kituo hicho utafanywa kesho siku ya Jumamosi Insha-Allah.

Kituo hicho ni sehemu ya upanuzi wa Darul-Hayaat kwenye mji tajwa, inayo tumika kupokea watu walio ambukizwa virusi vya Korona, kituo kina:

  • - Vyumba (56) kila chuma kina ukubwa wa (2m12).
  • - Vyumba (3) vya wahudumu wa afya kila chumba kina ukubwa wa (2m24).
  • - Chumba cha kubadilishia nguo wahudumu wa afya chenye ukubwa wa (2m6).
  • - Chumba cha kuwekea vifaa kinaukubwa wa (2m6).
  • - Sehemu ya mapokezi na ukumbi mkubwa wa wazi wenye ukubwa wa (2m1550).

Kumbuka kua mradi huu ni sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia sekta ya afya, aidha ni sehemu ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kulinda jamii na virusi vya Korona, ndipo mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wakaanza kazi ya ujenzi wa kituo hiki kwa kufuata maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, katika mji wa Imamu Hussein (a.s) hapa Karbala, na kusimamiwa na idara ya madaktari wa Ataba na hospitali ya rufaa Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: