Majibu kutoka ofisi ya Marjaa Dini mkuu kuhusu funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani pamoja na kusambaa kwa virusi vya Korona

Maoni katika picha
Leo siku ya Jumamosi mwezi 17 Shabani 1441h sawa na 11 Aprili 2020m limetoka jibu kuhusu funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu katika mazingira ya kusambaa kwa virusi vya Korona duniani.

Jibu hilo lilitokana na swali lililo ulizwa kuhusu funga ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Ifuatayo ni nakala ya jibu:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwengi wa rehema mwenye kurehemu.

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu na rehema zake pamoja na baraka zake

Mwezi mtukufu wa Ramadhani unakaribia na virusi vya Korona vinaendelea kusambaa katika miji tofauti, huku madaktari wakishauri kunywa maji mara kwa mara ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa virusi hivyo hatari, kwa sababu uchache wa maji mwilini unapunguza uwezo wa kinga ya mwili, na kukauka kwa koo kunarahisishia kirusi cha Korona kushambulia mfumo wa kupumua, wakati kunywa maji kunasaidia kuangamiza kirusi hicho, je wajibu wa kufunga mwezi wa Ramadhani utaondoka kwa waislamu mwaka huu kwa sababu hiyo?

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

Hakika ulazima wa kufunga mwezi wa Ramadhani ni wajibu kwa kila mtu, mtu yeyote aliyekamilisha masharti ya kufunga, lazima afunge bila kujali kuwajibikiwa kwa watu wengine au kutowajibikiwa, utakapo ingia mwezi wa Ramadhani ujao na muislamu akaogopa kufunga kwa sababu ya kuhofia kupata virusi vya Korona pamoja na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ulazima wa kufunga utaondoka kwake kwa sababu ya kuogopa kuambukizwa maradhi hayo, kama ataweza kupata matumaini ya kupunguza hofu ya kuambukizwa hata kama ikiwa ni kwa kukaa nyumbani na kuacha kuchanganyika na watu wengine au kwa kutumia barakoa (maski) na soksi za mikononi na vinginevyo, hautaondoka kwake wajibu wa kufunga.

Amma kuhusu yaliyosemwa kuwa madaktari wanashauri kunywa maji ili kujilinda na kupungua maji mwilini na kukauka koo –kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kujikinga na virusi vya Korona- hakuzuwii wajibu wa kufunga ispokua kwa yule ambaye hana njia nyingine kabisa ya kupunguza uwezekano wa kuambukizwa hata kwa kubakia nyumbani na kuchukua tahadhari zote tulizo taja, kinyume na hivyo ni lazima afunge.

Tambua kua unaweza kuepuka kupungukiwa maji mwilini ukiwa kwenye funga kwa kula mboga za majani na matunda yenye maji mengi, kama vile matango na matikiti maji kabla ya Alfajiri, pia unaweza kuepuka kukauka koo kwa kuweka mfuko wa plastiki mdomoni usiokua na kitu –kwa sharti ya kutofika kitu chochote kitokanacho na mfuko huo kooni- kuweka kitu mdomoni huongeza mate ambayo hayana tatizo lolote kuyameza ukiwa katika funga.

Kwa wale wasioweza kuacha kazi –kwa sababu yeyote- wakihofia kuambukizwa virusi vya korona kwa sababu ya kuacha kunywa maji mara kwa mara wakati wa mchana na wakawa hawana njia nyingine yeyote ya kujikinga na maambukizi hayo haitakua wajibu kwao kufunga, japokua haitafaa kudhihirisha kula kwao.

Ni wazi kuwa kufunga mwezi wa Ramadhani ni faradhi muhimu sana wala haifai kuacha bila udhuru wa kweli, na kila mwanaadamu anaitambua zaidi nafsi yake kama anaudhuru wa kweli wa kuacha kufunga au hana.

Kwa ufupi: Hakika wajibu wa kufunga katika michana ya mwezi wa Ramadhani huondoka kwa yule mwenye udhuru unaokubalika kisheria kama vile mgonjwa na mtu anaehofia kupata maradhi kama akifunga –kutokana na ushauri wa daktari- na akawa hana njia nyingine yeyote ya kujikinga na kupata maradhi hayo, ikipatikana njia ya kujikinga atalazimika kutumia njia hiyo na haitafaa kuacha kufunga.

Amani ya mwenyezi Mungu iwe juu yenu na rehema zake pamoja na baraka zake.

17 Shabani 1441h.

Ofisi ya Sayyid Sistani/ Najafu Ashrafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: