Kundi wa watumishi wa Ataba tukufu wa kiume na wakike wanaendesha program ya kugawa chakula kwa familia za mafakiri

Maoni katika picha
Katika kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia familia za mafakiri, kundi la watumishi wa Atabatu Abbasiyya katika Maahadi ya Turathi za Mitume (a.s) na masomo ya hauza, pamoja na chuo cha Ummul-Banina (a.s) cha kuandaa mubalighaat na kituo cha Alqamar, wanaendesha program ya kugawa chakula kwa familia za mafakiri kwenye mikoa tofauti.

Mkuu wa Maahadi ya turathi za mitume (a.s) Shekh Hussein Turabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kundi la wafanya kazi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kiume na wa kike, pamoja na wakufunzi na wanafunzi wa Maahadi ya turathi za mitume na chuo cha Ummul-Banina cha kuandaa mubalighaat na kituo cha Alqamar, wamejitolea sehemu ya mishahara yao na kununua chakula kwa ajili ya kwenda kugawa kwa familia za mafakiri kutokana na mazingira magumu ambayo taifa linapitia kwa sasa”.

Akaongeza kua: Idadi kubwa ya walimu na wanafunzi walikuwa wamesha toa vitu vya kusaidia, miongoni mwa vitu hivyo ni vyakula na dawa zilizo sambazwa kwa familia za mafakiri katika mikoa tofauti ya Iraq.

Kumbuka kua opresheni hii ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu aliye himiza kusaidia familia za mafakiri, wakati wa kipindi hiki cha marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: