Mawakibu za watu wa Qassim: Utowaji wetu unatokana na yule ambaye tunajivunia jina lake

Maoni katika picha
Wakazi wa mji wa Qassim (a.s) uliopo katika mkoa wa Baabil ni maarufu kwa kukirimu wageni na roho nzuri, sifa hizo zinaonekana sehemu nyingi, ikiwemo namna wanavyo wahudumia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s), kila mwaka mamilioni ya mazuwaru wa Arubaini au wanaokwenda katika malalo ya Qassim bun Imamu Mussa bun Jafari (a.s), utawakuta wanashindana kuwahudumia na kutoa kila wanacho miliki, kwa kweli wanaendeleza ukarimu wa wanaye mhudumia.

Mawakibu za mji huo zinamchango mkubwa katika mazingira haya ambayo taifa linapitia kwa sasa kama walivyo kua na mchango katika kusaidia majemedari wa Iraq wakati wa vita dhidi ya magaidi wa Daeshi, walijitolea nafsi na mali hadi ulipo patikana ushindi, leo wamekusanya nguvu na kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo wakati huu wa marufuku ya kutembea.

Kiongozi wa idara ambayo ipo chini ya kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Shekh Ahmadi Jubairi amesema kua: “Tulianza kutoa misaada tangu siku za kwanza yalipotolewa maelekezo ya Marjaa Dini mkuu, na bado tunaendelea hadi tatizo hili litakapoisha, tunawapa umuhimu mkubwa mafakiri na watu wenye kipato kidogo hakika tumesimama pamoja nao kwa kugawa mamia ya vikapu vya chakula kila siku”.

Akaongeza kua: “Mji wa Qassim (a.s) unajulikana kwa ukarimu wake na unajua tatizo lililopo, mawakibu zimeunganisha nguvu na kuunda vikundi vya kugawa misaada mfululizo, walianza kugawa kwenye vijiji vya mbali hadi katikati ya mji na maeneo ya pembezoni mwake, kwa namna ambayo inalinda heshima ya mtu anayesaidiwa, tumefanikiwa kugawa vikapu vya aina tofauti za vyakula, ambavyo vimesaidia kupunguza makali ya njaa japo kidogo katika kipindi hiki cha mtihani, bado tunaendelea kugawa.

Kumbuka kua ugawaji huo wa chakula ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu na kufuata maelekezo yake, aidha ni sehemu ya mradi wa Takaaful ulioanzishwa na kitengo cha Mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kupitia wawakilishi wake waliopo mikoani, kwa kusaidia mafakiri na watu weneye kipato kidogo wakati huu wa marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, Mawakibu za Husseiniyya bado zinaendelea kusaidia watu wenye uhitaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: