Maoni katika picha
Kiongozi wa uzalishaji wa bidhaa katika shirika hilo Ustadh Salaam Salamani amesema kuwa: “Shirika la Khairul-Juud baada ya kufanya utafiti linatarajia kutoa bidhaa yenye uwezo mkubwa wa kuuwa virusi na bakteria kwa bei nafuu watakayo weza kumudu watu wenye kipato kidogo”.
Akasisitiza kua: “Shirika linatarajia kuzalisha bidhaa hii mpya ambayo inaubora wa asilimia (%100) bidhaa hiyo ina (Peroxide ya heyrophodian) yenye uwezo mkubwa wa kuuwa virusi na bakteria”.
Akafafanua kua: “Bidhaa hiyo itakuwa katika ujazo tofauti na itauzwa kwa bei nafuu, kutakua na chupa za (lita 1) hadi (ml 100), aidha zitakuwepo chupa za (ml 500) na (ml 250)”.
Akaongeza kua: “Bidhaa hii ni nzuri kushinda bidhaa za zamani (Al-Ithanuul), kwa sababu zinauwezo mkubwa, akasisitiza kua haijachanganywa na kemekali zingine za ziyada”.
Kumbuka kua shirika la Khairul-Juud ni miongoni mwa miradi muhimu ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inatengeneza barakoa (maski) na visafishio (sabuni) vitu ambavyo vinahitajiwa na kila mtu kwa sasa, sambamba na taasisi za serikali katika kipindi hiki cha kupambana na virusi vya Korona.