Idara ya uhusiano wa vyuo na shule inatangaza matokeo ya shindano la hati bora ya kiarabu ya kuandika kwa mkono Duaau-Faraji

Maoni katika picha
Idara ya mahusiano ya vyuo na shule katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza matokeo ya shindano la hati bora ya kiarabu ya kuandika kwa mkono Duaau-Faraji: (Allahumma kun liwaliyyika Hujjatu bun Hassan swalawatuka alaihi wa alaa aabaaihi…).

Shindano hili lilikua na jumla ya washiriki (400) kwa hiyo kamati iliyo ratibu na kusimamia shindano hilo imeongeza idadi ya washindi kutoka (5) hadi (10) sambamba na kuongeza zawadi za washindi.

Washindi ni:

  • Mshindi wa kwanza: Azharu Sharikaau, kutoka jamhuri ya kiislamu ya Iran.
  • Mshindi wa pili: Mustafa Jaasim Muhammad, kutoka mkoa wa Waasit – Iraq.
  • Msindi wa tatu: Ayubu Mustafa Zaibili, kutoka mkoa wa Basra/ Chuo kikuu cha Basra cha mafuta na gesi.
  • Mshindi wa nne: Abdul-Adhim Khalili Yadikaar, kutoka mkoa wa Karkuuk – Iraq.
  • Mshindi wa tano: Aadil Khamisi Hassan, kutoka mkoa wa Karbala – Iraq.
  • Mshindi wa sita: Hussein Hassan, kutoka taifa la Kuwait.
  • Mshindi wa saba: Zaharaa Auda Adhabu, kutoka mkoa Dhiqaar – Iraq, chuo kikuu cha Dhiqaar/ kitivo cha utaktari.
  • Mshindi wa nane: Rahim Abdu-Boyo, kutoka mkoa wa Karbala – Iraq.
  • Mshindi wa tisa: Zainabu Auda Adhabu, kutoka mkoa wa Dhiqaar – Iraq, chuo kikuu cha Dhiqaar/ kitivo cha udaktari.
  • Mshindi wa kumi: Ahamadi Salim Ismaili, kutoka mkoa wa Najafu – Iraq.
  • Zawadi ya upendeleo kwa: Dada Laila Ghaanim Kharibti/ mwanafunzi wa darasa la kufuta ujinga hatua ya pili, kutoka mkoa wa Bagdad – Iraq.

Kumbuka kua idara ya mahusiano ya vyuo vikuu katika Atabatu Abbasiyya chini ya harakati za mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, imeendesha shindano la hati bora ya kiarabu ya kuandika kwa mkono Duaau-Faraji: (Allahumma kun liwaliyyika Hujjatu bun Hassan swalawatuka alaihi wa alaa aabaaihi…), kama sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa muokozi wa binaadamu Imamu Mahadi (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: