Ofisi ya Marjaa Dini mkuu inaiomba mahakama ya Iraq katika mkoa wa Baabil imuachie huru raia aliye hukumiwa kwenda jela kwa kosa la kumvunjia heshima Mheshimiwa

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu leo siku ya Jumatatu mwezi (19 Shabani 1441h) sawa na tarehe (13 Aprili 2020m) imemuandikia barua hakimu wa mahakama ya Hilla kumuomba amuachie huru mtu aliye hukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kumvunjia heshima Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani kwenye mitandao ya kijamii.

Barua imesisitiza kuwa; Mheshimiwa haridhii kuona mtu anaadhibiwa kwa sababu ya kumvunjia heshima, ameomba zichukuliwe hatua za kisheria haraka kwa ajili ya kumuacha huru.

Kwa taarifa zaidi angalia picha ya barua iliyo ambatana na habari hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: