Mawakibu za Karkha zimeongeza nguvu katika kuhudumia watu walio athirika na marufuku ya kutembea

Maoni katika picha
Kiongozi wa ofisi ya Karkha ambayo ipo chini ya kitengo cha mawakibu na vikosi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Shekh Muhammad Abadi, amesema kua mawakibu pamoja na wahisani wao wamejitolea kila walicho nacho kuzisaidia familia zilizo athirika na marufuku ya kutembea kwa ajili ya kuzuwia virusi vya Korona, hususan familia za mafakiri ambao hawamiliki mali za kutumia katika kipindi hiki, tumeandaa misafara tofauti ya kugawa misaada kama sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu, aliye himiza kusaidiwa familia hizo.

Akaongeza kua: “Tuliunda kamati maalum kwa ajili ya kutambua familia za wahanga wa marufuku ya kutembea tangu siku za kwanza za marufuku hiyo, na kuandaa chakula pamoja na vitu vingine kwa ajili ya familia hizo kulingana na uwezo wetu, kisha tukaweka vitu hivyo kwenye vikapu na kuanza kugawa kwa ndugu zetu wapenzi, kazi hiyo tumekua tukiifanya kila siku kutokana na wingi wa familia hizo, tunashirikiana na viongozi wa maeneo husika pamoja na Mu’tamad wa Marjaa Dini mkuu wa eneo husika, tulianza kwa kufanya msafara mmoja kwa siku lakini hivi sasa tunafanya zaidi ya msafara mmoja kwa siku, ili kuweza kuzifikia familia nyingi zaidi na kupunguza japo kidogo matatizo yao, tutaendelea kufanya hivi kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu hadi balaa hili litakapo isha”.

Kumbuka kua misafara hii ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu, pia ni miongoni mwa opresheni ya Hamlatu-Takaaful iliyo anzishwa na kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kupitia wawakilishi wake waliopo kwenye mikoa yote ya Iraq, kuzisaidia familia zilizo athirika na marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Korona, mawakibu hizo bado zinaendelea kusaidia familia hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: