Kikosi cha Abbasi kimeongeza nguvu katika harakati zake za kujikinga, na kimeanza kupuliza dawa katika mtaa wa Naqibu – Karbala

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kimeongeza nguvu katika kupambana na virusi vya Korona, ilianza kupambana na virusi hivyo tangu siku za kwanza kugundulika kwake, kikosi hicho kimeanza kazi ya kupuliza dawa katika mtaa wa Naqibu hapa Karbala, baada ya kumaliza kupuliza dawa kwenye mitaa mbalimbali ndani ya mkoa huu siku za nyuma.

Msemaji wa kikosi ameripoti kua wametumia gari kumi katika kupuliza dawa kwenye mtaa wa makazi wa Dauru katika juhudi za kupambana na virusi vya Korona, akasisitiza kua wana vifaa vyote vinavyo hitajika katika kazi hiyo.

Tambua kua kazi hii ilianza tangu siku za nyuma, na wameongeza juhudi baada ya Marjaa Dini mkuu kusisitiza ulazima wa kueshimu maelekezo ya wizara ya afya kujikinda na maambukizi ya virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: