Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimeanza kupuliza dawa katika mkoa wa Diwaniyya

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi), kimeanza opresheni ya kupuliza daya kwenye mitaa ya makazi ya watu, katika mikoa tofauti ya Iraq, ili kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, kikosi hicho kupitia opresheni ya Furat Ausat ya Hashdi Shaábi kimewasili katika mkoa wa Diwaniyya siku ya Jumatano na kuanza kupuliza dawa.

Msemaji wa kikosi ameripoti kua kikundi cha wapuliza dawa kimeanza kazi hiyo kwenye vitongoji tofauti na katika nyumba za makazi, kazi bado inaendelea.

Opresheni hii inatokana na maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliye himiza kufuata muongozo wa idara ya afya pia ni sehemu ya mkakati maalum wa kupambana na virusi vya Korona.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/ 26 Hashdi Shaábi) kwa kushirikiana na shirika la Khairul-Juud wanaendesha opresheni ya (Hamlatul-Atwaa) ya kupuliza dawa katika mitaa ya Karbala, ambayo ilianza siku ya Jumatatu (16 Machi 2020m) bado kazi hiyo inaendelea hadi sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: