Kituo cha uzalishaji wa vipindi na matangazo mubashara Alkfeel kimetoa filam fupi ya Marjaa wa taifa (Marjaiyyatu-Watwani)

Maoni katika picha
Kituo cha uzalishaji wa vipindi na matangazo mubashara chini ya kitengo cha habari, kimetoa filamu fupi iitwayo: Marjaa wa taifa (Marjaiyyatu-Watwan) inayo onyesha namna Marjaa Dini mkuu anavyo simama pamoja na raia wa Iraq katika mitihani tofauti iliyo likumba taifa hili.

Filam inaonyesha juhudi kubwa iliyo fanywa na Marjaa Dini mkuu na misimamo yake ya kihistoria katika kulinda taifa la Iraq na umoja wake, na namna alivyo kua mlezi wa raia wote bila kuangalia tofauti za mitazamo yao wakati wa matatizo yaliyo likumba taifa, misimamo yake imeleta mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na fatwa ya jihadi kifaya dhidi ya magaidi wa Daesh, na hatua zilizo fuata za kuwasaidia wapiganaji na wakimbizi.

Filamu inaisha kwa kuonyesha jambo la mwisho alilotolea maelekezo na bado anaendelea kulitolea ufafanuzi, tatizo la virusi vya Korona, kuanzia wito wake wa kuheshimu na kufuata maelekezo ya watalamu wa afya hadi fatwa aliyo sema kuhudumia wagonjwa wa Korona ni wajibu kifaya, pamoja na kuhimiza kusaidia watu wenye kipato kidogo na mafakiri, inaishia kwenye kuonyesha kazi inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kujenga vituo vya kuhudumia watu walio ambikizwa virusi vya Korona katika hospitali ya mji wa Imamu Hussein (a.s) kwenye mji wa Karbala, na katika mji wa Hindiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: