Mafundi wa kitengo cha wahandisi wanafunga mitambo ya kupuliza dawa katika hospitali ya Safeer, Alkafeel na katika mji wa Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wanafunga mitambo ya kupuliza dawa inayo fanya kazi yenyewe, katika hospitali ya Safeer, Imamu Hussein (a.s) na hospitali ya rufaa Alkafeel pamoja na mji wa Imamu Hussein (a.s), wanafanya hivyo kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.

Kiongozi wa kamati ya utendaji ya kitengo hicho, Mhandisi Mustafa Sa’adi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mtambo huo umetengenezwa kwa chuma na unasehemu maalum ya kutunzia kemikali pamoja na sehemu ya kupuliza maji”. Akaongeza kua: “Mtambo huo unapuliza watu na vifaa ili kuwalinda na maambukizi ya Korona”.

Dokta Mahadi Swahibu kiongozi wa idara ya kusimamia dawa katika hospitali ya rufaa Alkafeel amesema kua: “Mtambo huu unatumika kupuliza watu na vifaa, kama vile familia za wagonjwa na baadhi ya vifaa tiba kwa kutumia maji na dawa yenye uwezo mkubwa wa kuuwa bakteria na vairasi”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya imechukua hatua mbalimbali za kujikinga na virusi vya Korona, na inafuata maelekezo yote yanayo tolewa na wizara ya afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: