Chuo kikuu cha Al-Ameed kimegawa zaidi ya vikapu (200) kwa watu wenye kipato kidogo katika vitongoji vya Karbala

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed kimegawa vikapu vya chakula cha aina mbalimbali zaidi ya (200) kwa familia za mafakiri na wenye kipato kidogo ambao wameathiriwa na marufuku ya kutembea iliyopo katika mikoa ya Iraq pamoja na Karbala.

Vikapu vilikua na aina tisa za vyakula muhimu kwa familia, msaada huo ni muhimu sana katika mazingira ya sasa na wataendelea hadi tatizo litakapo isha.

Wanafanyia kazi maagizo ya Marjaa Dini mkuu kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa ya kupambana na virusi vya Korona.

Kumbuka kua Marjaa Dini mkuu alitoa wito wa kuunganisha nguvu katika kusaidia familia za mafakiri na watu wenye kipato kidogo, wakati huu wa marufuku ya kutembea kwa ajili ya kupambana na virusi vya Korona, ndipo Atabatu Abbasiyya ikaanzisha opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) ya kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: