Shuhudia kwa picha: opresheni kubwa zaidi ya kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo (Atakaaful) iliyo ratibiwa na mawakibu za soko la wazee (Suuqu-Shayuukh)

Maoni katika picha
Mawakibu za soko la wazee (Suuqu-Shuyuukh) katika mkoa wa Dhiqaar chini ya usimamizi wa Mu’tamadi Marjaiyya, zimeratibu opresheni kubwa ya kusaidia familia za wahanga wa marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Korona ambayo wameiita (Takaaful) kwa sababu ni sehemu ya opresheni zilizo tangulia na zingine zitaendelea, katika kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu aliyehimiza kusaidia watu wenye kipato kidogo ambao wameathiriwa na marufuku ya kutembea.

Hayo yamesemwa na kiongozi wa mawakibu Husseiniyya katika wilaya hiyo ambazo zipo chini ya kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Aqiil Turki, amesema: Opresheni hii ni sehemu ya kutekeleza wajibu wa kidini, kitaifa na kibinaadamu, kupitia wito wa Marjaa Dini mkuu wa kuunganisha nguvu, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na moyo wa wajumbe wa mawakibu Husseiniyya za wilaya hii pamoja na wahisani, wamejitolea vitu mbalimbali katika kipindi hiki kigumu, hiyo ndio desturi yao, pamoja na changamoto nyingi walizo nazo, wamejitolea kama walivyo jitolea wakati wa kupambana na magaidi wa Daesh, kwa mara nyingine wameonyesha moyo wa kibinaadamu wa hali ya juu.

Akaendelea kusema: “Tumeandaa maelfu ya vikapu vya chakula cha aina mbalimbali zinazo hitajiwa na familia nyingi kwa sasa, tumekiweka kwenye masanduku maalum, kutokana na wingi wake tumetumia uwanja wa michezo kukusanya masanduku hayo na kuyagawa kwa wastahiki, chini ya utaratibu maalum ulio andaliwa na kuhakikisha familia zote zilizo sajiliwa zinapata, tutaendelea kugawa misaada kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu hadi balaa hili litakapo isha”.

Kumbuka kua opresheni hii ni sehemu ya kuitikia wito wa Marjaa Dini mkuu pia ni miongoni mwa mkakati wa Takaaful ulioa anzishwa na kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kupitia wawakilishi wao wa mikoani, wa kusaidia familia zilizo athiriwa na marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, bado mawakibu Husseiniyya zinaendelea kusaidia familia zenye uhitaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: