Idara ya shule za wasichana za Alkafeel imetangaza majina ya washindi wa shindano la (Njia ya uwokovu)

Maoni katika picha
Idara ya shule za wasichana za Alkafeel leo siku ya Alkhamisi mwezi (22 Shabani 1441h) sawa na tarehe (16 Aprili 2020m) imetangaza majina ya washindi wa shindano la (Njia ya uwokovu) la kwanza kufanywa kwa njia ya mtandao na linalo husu wasichana peke yake, ambalo lilikua sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Mahadi (a.f), shindano lilikua na maswali ya Fiqhi, Aqida na masomo mengine, lililo anza siku ya Ijumaa mwezi (16 Shabani 1441h) na likaendelea kwa muda wa siku tano.

Jumla ya wasichana (929) kutoka ndani na nje ya Iraq wameshiriki kwenye shindano hilo, washiriki (314) wametoa majibu sahihi, ikabidi tupige kura kwa njia ya mtandao ili kupata washindi hamsini, pia kulikua na zawadi maalum kwa washiriki wote ambayo ni kuwafanyia ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa niaba pamoja na Duaau-Tawasul na Ziyaratu-Ashura, pamoja na kutoa nakala ya msahafu mtukufu na picha ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) iliyo andikwa jina la mshindi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: