Zaidi ya vikapu (3000) vya chakula vinatolewa na mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa askari wanaosimamia utekelezwaji wa marufuku ya kutembea

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imegawa zaidi ya vifurushi (3000) vya chakula kwa askari wanaosimamia utekelezaji wa marufuku ya kutembea kwa ajili ya kuzuwia maambukizi ya virusi vya Korona, kama sehemu ya kuonyesha kujali kazi wanayo fanya, ugawaji wa chakula unafanywa kwa wiki ya pili mfululizo.

Ugawaji wa chakula ni sehemu ya huduma za kibinaadamu zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya katika kupambana na virusi vya Korona.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa kitengo cha mgahawa (mudhifu) Mhandisi Aadil Hamami, amesema: “Kutokana na maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya, ya kusaidia askari wa aina zote ambao wako chini ya wizara ya ulinzi na mambo ya ndani, wanao simamia utekelezwaji wa marufuku ya kutembea kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Korona, bado watumishi wa mgahawa wanaendelea kugawa chakula kwa askari waliopo vituoni na wale wanao zunguka na gari katika mkoa wa Karbala”.

Akabainisha kua: “Chakula hicho hupikwa ndani ya jiko la mgahawa, halafu huwekwa kwenye vifungashio (take away), pamoja na matunda na maziwa, kuna gari maalum za kusambaza chakula”.

Kamanda wa polisi mkoa wa Karbala Ahmadi Ali Zawini amemshukuru mlinzi mkuu wa taifa letu Marjaa Dini mtukufu, namna anavyo wajali na kuwasaidia raia wote wa Iraq bila ubaguzi, pamoja na kuzishukuru Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya na watumishi wote wa Ataba hizo, kutokana na kazi kubwa wanayo fanya ya kupambana na tatizo la Korona, akasema kua tumezowea kuwaona wakiwa mstari wa mbele katika kutoa misaada kipindi chote cha matatizo yanayo likumba taifa letu, akamaliza kwa kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufu aliokoe taifa hili na maradhi ya Korona hakika yeye ndio mtegemewa na ndio muokozi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: