Muungano wa maktaba za kimataifa na taaluma (Ifla) umeingiza kisa cha maktaba na daru makhtutwaat kwenye mtandao wake maalum

Maoni katika picha
Muungano wa maktaba za kimataifa na taaluma (Ifla) umeingiza kisa cha maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye mtandao wake maalum, katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, imekua maktaba ya kwanza kuingizwa kisa chake katika mtandao huo.

Makamo kiongozi wa kituo cha faharasi na elimu Ustadh Samiri Baasim amesema kua: “Kituo cha faharasi na elimu kimefanyia kazi malengo mawili ya mkakati wa maendeleo endelevu ambayo ni lengo la (9) na lengo (11), hii ni hatua ya kwanza kuandikwa kisa cha maktaba kwenye mtandao wake”.

Akaongeza: “Kisa cha maktaba na daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeingizwa katika mtandao wa muungano wa maktaba za kimataifa (Ifla) katika kufanyia kazi mpango wa malengo endelevu chini ya anuani isemayo: (Kuhami turathi za kifikra na kuzifikia)”.

Akasema: “Hili ni tukio la kwanza kwa Iraq, maktaba na daru Makhtutwaat ya Ataba tukufu ndio ya kwanza kuingizwa kwenye mtandao huo miongoni mwa maktaba za taifa letu, Iraq imekua nchi ya pili katika nchi za kiarabu na ya kumi na sita katika nchi wanachama za muungano wa maktaba za kimataifa (Ifla)”.

Tambua kua haya ni mafanikio ya taifa la Iraq kwenye sekta ya maktaba na taaluma kimataifa, yamelifanya taifa hili kuingia katika mataifa yaliyo endelea na yanayo fanyia kazi malengo ya maendeleo endelevu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: