Kazi ya kupuliza dawa katika majengo ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea

Maoni katika picha
Kazi ya kupuliza dawa inayo fanywa na kamati ya kujikinga na maambukizi ya korona iliyo undwa na Atabatu Abbasiyya bado inaendelea chini ya utaratibu maalum walio jipangia, kwa ajili ya kudhibiti hatari ya virusi vya Korona.

Miongoni mwa sehemu za Atabatu Abbasiyya zinazo pulizwa dawa hiyo ni majengo ya kutolea huduma kwa mazuwaru kama vile mahoteli na sehemu zingine, wanatumia fursa ya sehemu hizo kuwa tupu, dawa inapulizwa kwa kufuata ratiba maalum iliyo pangwa na kikosi chenye vifaa bora vilivyo pasishwa na idara ya madaktari wa Ataba, ambavyo wamepewa na shirika la Khairul-Juud, wamepuliza dawa sehemu zote za majengo hayo, kuanzia kwenye kumbi, vyumbani, kwenye korido, kuta za ndani na nje na njia zinazo elekea kwenye majengo hayo na katika sehemu za bustani.

Kiongozi wa idara ya madaktari katika Ataba tukufu Dokta Osama Abdulhassan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tangu tulipo unda kamati ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, tumetengeneza mpango kazi unao husisha sehemu tofauti, lengo kuu ni kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona kwa kufuata maelekezo yaliyo tolewa na wizara ya afya ya Iraq pamoja na shirika la afya la kimataifa, miongoni mwa kazi tunazo fanya ni upuliziaji wa dawa endelevu”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu inautaratibu maalum wa kupuliza dawa uliopangwa na kamati ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, inayo husika na kupuliza dawa kwenye majengo ya Ataba, mji mkongwe na barabara za mkoa huu (Karbala).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: