Wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) katika mji wa Karkuuk wamekamilisha kazi ya kupuliza dawa

Maoni katika picha
Wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) wamekamilisha kazi ya kupuliza dawa katika mkoa wa Karkuuk, wamepuliza dawa maofisini, kwenye majengo ya taasisi, katika husseiniyya, misikiti, barabara, viwanja vya wazi na katika hospitali ya Karkuuk.

Wawakilishi wa kikosi wamesema kua: “Kazi hiyo imefanywa kwa kushirikiana na idara ya afya ya Karkuuk pamoja na jeshi la wananchi na idara ya maji ya Karkuuk, ilianza tangu tarehe (16/03/2020m) hadi tarehe (17/04/2020m)”.

Akasema kua wametumia pampu za mikono ambazo zinatumia betri za umeme, wamefanya kazi hiyo kwa juhudi kubwa, chini ya maelekezo ya viongozi wa kikosi katika kusaidia juhudi za serikali za kupambana na virusi vya Korona.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kilianza kupuliza dawa katika mkoa wa Karbala kwa kushirikiana na shirika la Khairul-Juud kupitia (Hamlatul-Atwaa) na bado wanaendelea hadi sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: