Viongozi wa Ataba tukufu wanafuatilia kwa karibu shughuli za ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika hospitali ya Hindiyya

Maoni katika picha
Makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi, asubuhi ya Jumapili mwezi (25 Shabani 1441h) sawa na tarehe (19 Aprili 2020m) ametembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona kinacho jengwa katika hospitali ya wilaya ya Hindiyya kusini mwa mkoa wa Karbala, unao tekelezwa na mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Amefuatana na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na viongozi wemgime, na mkuu wa idara ya afya ya Karbala, wameangalia maendeleo ya kazi pamoja na kiwango cha ukamilifu.

Rais wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya Shekh Swalahu Khafaji ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi wanafanya kazi kama nyuki, kinacho onekana katika mradi huu ndio uhalisia wa juhudi na uamimifu wa wafanyakazi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), wanakumbusha jinsi wairaq walivyo itikia wito wa fatwa ya kujilinda iliyo tolewa na Marjaa Dini mkuu kwa ajili ya kupambana na magaidi wa Daesh”.

Kumbuka kua mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya walianza kazi ya ujenzi wa kituo cha kuhudumia watu walio ambukizwa virusi vya Korona tangu mwezi (6 Shabani 1441h) sawa na tarehe (31 Machi 2020m), kituo hiki kinajengwa katika kiwanja chenye ukubwa wa (2m1500) na kinavyumba (35) pamoja na chumba cha usafi na cha dawa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: