Kwa video: Shughuli za usafi na kupuliza dawa zinafanywa na wahudumu wa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kujikinga na janga la Korona

Maoni katika picha
Wahudumu wa kitengo cha utumishi na wale wa kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu wameanza kazi ya kusafisha eneo lote linalo zunguka Ataba pamoja na ukuta wa jengo tukufu la Ataba, kazi hiyo ni sehemu ya mkakati wa kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona.

Makamo rais wa kitengo kinacho simamia eleo la katikati ya haram mbili tukufu Ustadh Qassim Awadi, amesema kua: “Tumejikita katika kusafisha eneo la katikati ya haram mbili na maeneo yanayo zunguka haram hizo pamoja na barabara zote zinazo elekea Ataba takatifu, halafu sehemu hizo zitapulizwa dawa”.

Kiongozi wa idara ya kusafisha jengo Ustadh Qassim Muhammad amesema kua: “Kuna watumishi wanafanya kazi kwa zamu tatu, yani kazi inafanywa saa (24) bila kupumzika, wanafagia, wanapiga deki na kupuliza dawa”.

Wanatumia vifaa vilivyo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud chini ya usimamizi wa kamati maalum inayo husika na kujinga na virusi vya Korona iliyo undwa na Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya imefanya mambo mengi kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Korona, inatekeleza na kufuata maelekezo ya idara ya afya, katika ngazi ya Ataba, mji mkongwe na mkoa kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: