Hospitali ya Alkafeel imeingiza mtambo wa kisasa wa kutibu maradhi ya ubongo

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel imeingiza mtambo wa kisasa wa kutibu maradhi ya ubongo kwa kutumia mionzi uutwao (Periscope of nervous system diseases), mtambo huo utasaidia kupunguza visa vya uparuaji, kuletwa kwa mtambo huo ni sehemu ya juhudi zinazo fanywa na Ataba za kununua vifaa tiba vya kisasa, ili kutoa huduma bora za afya kwa raia wa taifa hili.

Kwa mujibu wa maelezo ya Dokta Saamir Fasal daktari wa upasuaji katika hospitali hiyo, amesema: kuletwa kifaa hicho ni sehemu ya mkakati maalum wa kuboresha huduma za afya na vifaa tiba, mtambo huo ni sehemu ya mitambo muhimu inayo hitajika katika chumba cha upasuaji, nacho ni kifaa cha kisasa zaidi katika tiba ya maradhi ya ubongo.

Akaongeza kua: “Miongoni mwa matumizi ya mtambo huo ni kuondoa uchafu kwenye ubongo na kutibu sehemu zenye madhara kwenye ubongo, pamoja na upasuaji wowote ambao hufanywa kwenye njia ya pua pamoja na sehemu za shingoni kwa mbele na nyuma, ikiwa ni pamoja na sehemu za kifuani, tumboni na mgongoni”.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali tembelea mtandao wa hospitali ufuatao: (www.kh.iq) au piga simu kwa namba zifuatazo: (07602329999) au (07602344444).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: