Maahadi ya Quráni tukufu imetangaza program ya mwezi mtukufu wa Ramadhani

Maoni katika picha
Mkuu wa Maahadi tukufu katika Atabatu Abbasiyya Shekh Jawadi Nasrawi ametangaza kukamilika kwa program ya Quráni itakayo fanywa katika mwezi wa Ramadhani chini ya utaratibu wa kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, kama ilivyo elekezwa na kamati ya kujikinga na maambukizi.

Akabainisha kua: “Program ya Quráni mwaka huu itakua na vitu vifuatavyo:

  • - Usomaji wa Quráni Tartiil ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kurushwa kwenye vyombo vya habari sambamba na kuzingatia kutokuwepo kwa mkusanyiko (kukurubiana).
  • - Ratiba ya meza ya vizito viwili (Maaidatu-Thaqalaini) ambayo ni mashindano ya vikundi sita yataratibiwa kupitia mitandao ya kijamii na watu kutoka mikoa tofauti watashiriki.
  • - Kufundisha somo la maarifa ya Quráni kwa hatua mbalimbali”.

Nasrawi akasisitiza kua: Program yote itazingatia tahadhari za kiafya, na kufuata maelekezo yote kuhusu kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, ikiwa ni pamoja na kujiepusha na mikusanyiko.

Akafafanua: Atabatu Abbasiyya itaendesha program tofauti katika mwezi wa Ramadhani, sambamba na kufuata maelekezo yote kuhusu kujikinga na virusi vya Korona, program ya usomaji wa Quráni tukufu itarushwa kwenye vituo kadhaa vya luninga (tv), kufanya hivyo ni sehemu ya kuzishirikisha familia kwenye ratiba hiyo takatifu ndani ya mwezi mtukufu katika mazingira haya magumu ambayo taifa linapitia kwa sasa.

Kumbuka kua Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya imezowea kuendesha program mbalimbali za Quráni kila mwaka, lakini kutokana na mazingira ambayo taifa linapitia kwa sasa na kutokana na tahadhari zinazo chukuliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, imelazimika kupunguza baadhi ya program.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: