Shamba boy wa Alkafeel wameanza kupanda mauwa ya msimu

Maoni katika picha
Kikosi cha shamba boy wa Alkafeel kinaendelea na kazi yake ya kuhakikisha kinapamba Ataba na maeneo yake kwa mauwa ya aina tofauti, hiyo ni sehemu ya shughuli zake katika mwaka, tayali kimesha leta miche ya mauwa yaliyo oteshwa kwenye vitalu vyake.

Kazi ya kuweka miti ya mauwa hufanywa kwa utaratibu maalum uliopangwa na jopo la wataalamu, kama ilivyo elezwa na kiongozi wa idara ya kilimo Mhandisi wa kilimo Mustafa Hassan Haadi: “Shamba boy wa Alkafeel wamekamilisha maandalizi ya msimu wa kiangazi ya kuipatia Atabatu Abbasiyya na vitengo vyake aina mbalimbali za miti ya mauwa ambayo huoteshwa kwenye vitalu vyetu, katika msimu huu tunazaidi ya miche (700) ya aina tofauti ambayo tutaigawa kwa Ataba tukufu na vitengo vyake kulingana na mahitaji yao, na sehemu nyingine watapewa wenye vitalu”.

Akabainisha kua: “Kazi nyingine ya shamba boy hao ni kupanda miti ya mauwa kwenye barabara, hupandwa maelfu ya miti katika msimu mmoja, shamba boy wa Alkafeel hawajajifunga sehemu moja, wanahudumia sehemu tofauti na kuhakikisha mji wa Karbala unakua wa kijani kibichi”.

Kumbuka kua shamba boy wa Alkafeel hupanda miti ya mauwa ya msimu na isiyokua na msimu, miti ya mauwa na ya kivuli sambamba na kuendelea kuihudumia kitaalamu chini ya wabobezi wa maswala hayo, jambo ambalo limefanya wawe na maendeleo makubwa katika sekta hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: