Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinaendelea kupuliza dawa katika mkoa wa Karbala

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji (Liwaau/26 Hashdi Shaábi) kinaendelea na kazi ya kupuliza dawa katika mitaa ya Karbala chini ya usimamizi wa kamati ya kupambana na korona.

Msemaji wa kikosi ameripoti kua: kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kinaendelea na kazi ya kupuliza dawa katika mji wa Karbala, tayali wamepuliza dawa katika mtaa wa Jumuiyya na Mukhayyam, wametumia lita (6000) za dawa kwenye eneo lenye ukubwa wa kilometa (8 – 10).

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) kinaendelea kuwahudumia wananchi kwa kushiriki katika opresheni ya (Marjaiyyatu-Takaaful) au kupuliza dawa kwenye mikoa mbalimbali ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: