Idara ya magodauni imeongeza juhudi ya kugawa vifaa vya kujikinga na maambukizi kwenye vituo vyote vya Ataba tukufu.

Maoni katika picha
Idara ya magodauni chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya inagawa barakoa na vifaa vingine vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona kwenye vitengo vyote vya Atabatu Abbasiyya.

Kiongozi wa idara hiyo Ustadhi Haidari Abbasi Hussein ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Katika mazingira ya kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya Korona ni jukumu letu kugawa vifaa vya kujikinga na maambukizi kwenye vituo vyote vya Atabatu Abbasiyya vya ndani na nje”.

Akaongeza kua: “Kila siku tunagawa karibu barakoa (3000) na idadi sawa na hiyo ya soksi za mikononi, sambamba na kutoa lita (300) za dawa ya kuuwa bakteria kwa vitengo hivyo”.

Akasema: “Aidha tumeweka barakoa kwenye vituo tofauti vya afya pamoja na nguo za kidaktari na soksi za mikononi, na tumeandaa maeneo kadhaa kwa ajili ya kuhifadhi watu walio ambukizwa virusi vya Korona”.

Akafafanua kua: “Kazi zetu haziishii kwenye mkoa wa Karbala peke yake, tumesafirisha maelfu ya barakoa na vifaa vingine katika mikoa ya Baabil na Waasit”.

Kumbuka kua idara ya magodauni ni moja ya sehemu za kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: