Idara ya wanawake inafanya nadwa kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Idara ya wanawake imefanya nadwa ya tatu kwa njia ya mtandao, ambapo wamejadili nafasi ya vyombo vya hapari katika kupambana na Korona, nadwa hii ni sehemu ya kuangazia tatizo la Korona katika nyanja zote kielimu.

Nadwa imefanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (vyombo vya habari na kujenga uwelewa kwenye jamii kuhusu tatizo), yakajadiliwa mambo matatu yafuatayo:

Kwanza: nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga muelekeo wa taifa kuhusu tatizo la Korona.

Pili: nafasi ya vyombo vya habari vinavyo milikiwa na Ataba.. na athari ya viongozi wa Ataba kutembelea wahudumu wa afya na wahanga wa Korona.

Tatu: uwelewa wa jamii kuhusu swala hili kwa kupitia mitandao ya mawasiliano ya kijamii.

Nadwa imeongozwa na Dokta Raaida Kaadhim Fayaadh ambaye amebainisha nafasi ya vyombo vya habari katika kutatua tatizo, akafafanua kua vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kujenga uwelewa katika jamii na huitwa ni utawala wa nne.

Ustadhat Aamali Fatalawi kutoka ofisi ya kuazimisha vitabu katika idara ya maktaba ya wanawake chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu amesema kua: “Tumechagua mada ya (vyombo vya habari vya Ataba tukufu.. na uwepo wa viongozi wanaojenga uwelewa wa kiafya katika jamii kutokana na tatizo la Korona), kutokana na mchango wao mzuri kwenye kupambana na Korona, tumezungumza nukta muhimu katika kueleza hali halisi kwa ujumla, kisha tukaeleza nafasi ya Marjaa mkuu katika swala hili, na nafasi ya vyombo vya habari vya Ataba kwenye sekta tofauti, halafu tukajikita katika muongozo wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya pamoja na katibu wake mkuu na jinsi wanavyo kwenda kuangalia utendaji wa kazi na kutoa hamasa sambamba na kuwatia moyo wanajamii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: