Mradi wa kupuliza dawa unaoendelea ili kupambana na kusambaa kwa virusi vya Korona

Maoni katika picha
Kikosi cha kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona kilicho undwa na Atabatu Abbasiyya kinaendelea na mradi wa kupuliza dawa katika jitihada ya kupambana na kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya Korona.

Kiongozi wa idara ya madaktari wa Atabatu Abbasiyya Dokta Osama Abdulhassan na wajumbe wa idara hiyo wameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tangu kilipo undwa kikosi cha kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona tuliweka ratiba yenye vipengele vingi, lengo kuu likiwa ni kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona chini ya kanuni na muongozo wa wizara ya afya ya Iraq na shirika la afya la kimataifa, miongoni mwa ratiba hiyo ni kazi ya kupuliza dawa katika jengo la Ataba na maeneo yote yanayo zunguka Ataba ikiwa ni pamoja na miradi inayo endelea kutekelezwa hivi sasa”.

Kiongozi wa idara ya ujenzi katika kitengo cha usimamizi wa kihandisi na msimamizi wa utekelezaji wa miradi hiyo Ustadh Hassan Ali Abdulhussein amesema kua: “Tunaendelea kupuliza dawa sehemu zote za Atabatu Abbasiyya, ikiwa ni pamoja na miradi inayo jengwa hivi sasa, tunapuliza dawa kwenye kila mradi, pamoja na vyumba vya ofisi na vituo vya afya”.

Akaongeza kua: “Tunatumia vifaa vilivyo idhinishwa na vinavyo endana na sehemu husika, tulivyo pewa na shirika la Khairul-Juud, visivyo kua na athari kwa afya ya mwanaadamu na salama kwa ujumla, tunafanya kazi kwa kufuata maelekezo ya wahusika”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kujikinga na virusi vya Korona, sambamba na kufanyia kazi muongozo wa kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona unaotolewa na wizara ya afya katika ngazi ya Ataba, mji mkongwe na mkoa kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: