Chuo kikuu cha Al-Ameed kinaratibu na kuendesha semina na warsha kwa njia ya masafa (mtandao).

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza semina na warsha kwa njia ya masafa (online) kwa watumishi na kila anayependa kushiriki, ratiba hiyo inatokana na kufungwa shule za serikali na binafsi kwa sababu ya janga la Korona.

Mkuu wa kitengo cha elimu endelevu Dokta Aqiil Alaa Hussein ambaye kitengo chake kinashirikiana na kituo cha kompyuta, wanasimamia uratibu na uwendeshaji wa semina na warsha hizo amesema kua: “Chuo kimefanya kila kiwezalo kuandaa warsha na semina, ili kuhakikisha harakati za elimu hazisimami, pamoja na kufuata muongozo wa rais wa chuo katika kuendesha semina na warsha kama ilivyo kuwa kwenye ratiba ya awali, ilimradi chuo kiendelee kutoa elimu hadi kwenye mazingira magumu kama haya ambayo taifa linapitia kwa sasa”.

Kumbuka kua tangu kuanza kwa janga hili la kitaifa na kimataifa, chuo kimekua mstari wa mbele kufuata maelekezo yote ya kiafya yanayo tolewa na wizara ya afya ya Iraq pamoja na shirika afya la kimataifa kuhusu kujikinga na virusi vya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: